Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mwakyembe Amtaka Mhandisi wa Jengo la Wizara Kuongeza Juhudi Kukamilisha Kazi

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Hagay Mziray Mzinga Holding Company Ltd ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo la wizara kwa kumtaka aongeze juhudi ili waweze kumalizi kazi hiyo kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya wizara unaondelea katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

Na Anitha Jonas – WHUSM Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe amemtaka Mhandisi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali kuongeza juhudi ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Mheshimiwa  Mwakyembe ametoa maagizo hayo usiku wa kuamkia Februari 11,2019 alipofanya ziara yake katika eneo hilo panapojengwa katika Ofisi za Wizara eneo la Ihumwa Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo na kasi ya utendaji kazi kwa masaa ishirini na nne ili  kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliyopangwa.

“Kwanza nawapongeza kwa jitihada mnazozionyesha kwa kuifanya kazi hii kwa masaa ishirini na nne na kwa kazi mliyokwisha kuifanya mpaka sasa, ila nataka niwasisitize kuwa mnahitaji kuongeza juhudi zaidi ili muweze kumaliza ndani ya muda uliyopangwa na mjue kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu anatarajia kuja kukagua ujenzi huu hivi karibuni,hivyo basi mkumbuke mlimwaahidi nini kwani atahitaji mkamilishe ahadi  mliyompa,” alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Hagay Mziray (kulia) kutoka Kampuni ya Mzinga Holding Company Ltd alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua walizofikia katika ujenzi wa ofisi hiyo ya Wizara,usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 wakati Mheshimiwa Waziri huyo alipotembelea eneo hilo la ujenzi kufuatila utendaji kazi na kasi ya ujenzi ya ofisi hiyo unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni, katika Mji wa Serikali uliyopo eneo la Ihumwa Jijini Dodoma,wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akikagua ndani ya jengo la ofisi ya wizara ujenzi unaoendelea na hatua zilizofikiwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019,alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo na kuhakiki utakelezaji wa shughuli hizo za ujenzi kwa masaa ishirini na nne.

Naye Mkandarasi Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi za Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoka Kampuni ya Mzinga Holdings Company Ltd Mhandisi Hagay Mziray alimweleza Mheshimiwa Waziri Mwakyembe kuwa kwa sasa kazi zinazoendelea ni pamoja na upakaji wa rangi nyeupi kabla ya kupaka rangi,usimikaji wa mabomba ya vyoo na  umeme na wanatarajia kufunikia chemba za maji taka  pamoja na shughuli nyingine mbalimbali.

“Hatua ya ujenzi wa jengo  ilipofikia kwa sasa ni sawa na majengo mengine ya ofisi za wizara mbalimbali yaliyopo katika Mji huu wa Serikali kwa sasa na wote tunajitahidi kukamilisha kazi hii kwa wakati, ila kufuatia changamoto mbalimbali tuliandika barua ya kuomba kuongezewa siku za kukabidhi jengo hili kuweza kuwa Februari 28,2019 badala ya Februari 15,2019,”alisema Mhandisi Mziray.

Akiendelea kuzungumza  Mhandisi Mziray alisema pamoja na hapo awali jengo hilo kuonekana kuwepo nyuma katika ujenzi wake kwa sasa hatua walizofikia ni nzuri na hatua wanayoelekea kwa sasa ni ukamilishaji wa ujenzi huo ikiwemo kupaka rangi na kuanza kuweka tiles na kuweka celing board.

Halikadhalika nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Bibi. Prisca Shewali alimsitisiza mhandisi huyo kuhakikisha wanafunika mashimo hayo ya maji taka kwa zege haraka ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutona na shughuli nza ujenzi zinazoendelea mahali hapo.

 

One thought on “Waziri Mwakyembe Amtaka Mhandisi wa Jengo la Wizara Kuongeza Juhudi Kukamilisha Kazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama