Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kilele cha Maadhimisho Siku ya UKIMWI

Na;  Frank Mvungi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim   Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhisho ya siku ya UKIMWI yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dodoma  Desemba  Mosi 2018.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho  ya siku hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri  Mkuu anayeshughulikia Walemavu Mhe. Stella   Ikupa  amesema kuwa maadhimisho hayo yatatanguliwa na matukio mbalimbali yatakayoanza tarehe 24 Novemba 2018.

“ Matukio mbalimbali yatakayofanyika katika kuadhimisha siku hii ni pamoja na Maonyesho ya Shughuli za wadau wa kudhibiti Virusi vya UKIMWI, Kongamano la Kitaifa la kutathmini hali ya mwelekeo wa kudhibiti  Virusi vya UKIMWI litakalofanayika tarehe 27 na 28 mwezi Novemba, 2018’’; Alisisitiza Mhe. Ikupa

Akifafanua amesema kuwa wananchi wa mikoa ya jirani wanakaribishwa kushiriki katika maadhimisho kuanzia tarehe 24.

Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yametoa kipaumbele kwa masuala yanayohusu vijana kwa kutambua kuwa vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi na pia asilimia 40 ya maambukuzi mapya ya Virusi vya UKIMWI hutokea kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.

 Katika maadhimisho hayo yatakayoanza tarehe 24 Novemba, 2018 jumbe mbalimbali zitatolewa kwa ajili ya kufikisha elimu ya VVU na UKIMWI kwa vijana wa Vyuo Vikuu, Sekondari, Shule za Msingi na Vijana walio nje ya shule.

Akizungumzia  ushiriki wa wadau mbalimbali amesema kuwa yatashirikisha wageni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wadau wa Maendeleo, sekta binafsi na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, viongozi wa dini, asasi za kiraia.

Maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanatoa fursa ya kutathmini hali halisi na mwelekeo wa idhibiti wa UKIMWI na vilevile kubaini changamoto, mafanikio na mikakati mbalimbali katika kupambana na janga hili. Siku hii pia inatoa nafasi ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na janga la UKIMWI na kuwajali yatima waliotokana na janga hili.

162 thoughts on “Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kilele cha Maadhimisho Siku ya UKIMWI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama