Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mpango wa Pili Jumuishi wa Huduma za Kifedha

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu leo jijini Dar es Salaam.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndullu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Gavana Mteule wa BOT, Profesa Florens Luoga.

Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba za viongozi mbambalimbali.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya kuzindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)

68 thoughts on “Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mpango wa Pili Jumuishi wa Huduma za Kifedha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama