Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akagua Miche Mipya ya Korosho

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiangalia Mche Mpya wa Korosho, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa Miche Mipya ya Korosho kutoka kwa Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Tanzania, Domina Mkangara, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Hassan Jarufu, wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Desemba 31, 2017. Katikati ni Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Domina Mkangara

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho aliyoupanda, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi mche mpya wa mkorosho Bi. Mwanahamisi Saidi, mkazi wa Kilimahewa, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama