Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Azindua Kituo cha Huduma za Utalii Wilayani Karatu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa bwana Francis Theodosia.

161 thoughts on “Waziri Mkuu Azindua Kituo cha Huduma za Utalii Wilayani Karatu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama