Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu asisitiza Michezo ni Ajira

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja mshindi wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali  kuendelea kuviendeleza kwakua Michezo katika Dunia ya leo ni ajira.

Mhe.Waziri Mkuu ameyasema hayo hivi karibuni Jijini Arusha katika Mashindano ya Riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyolenga kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine aliefariki miaka 35 iliyopita ambapo ameeleza kuwa marehemu Sokoine alikua anapenda sana michezo pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

“Michezo ni muhimu kwakua inaleta umoja,ushirikiano furaha lakini zaidi katika dunia ya leo ni ajira ya kuaminika hivyo ni lazima vijana mkatumia vipaji mlivyonavyo katika michezo mbalimbali ili muweze  kupata ajira na hatimaye mfanikiwe kama wengine waliofanikiwa kupitia sekta hii”.alisema Mhe.Kassim Majaliwa.

Aliongeza kuwa Michezo kwa sasa inatangaza Taifa letu ambapo ametolea mfano wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo hivi karibuni imefuzu kushiriki Michuano ya AFCON itakayochezwa baadae mwezi juni huko nchini Misri,Timu ya Vijana chini ya Miaka 17 “Serengeti Boys” itakayoshiriki Mashindano hayo ambayo yatafanyika hapa nchini kuanzia April 14 -28 mwaka huu ambapo timu hiyo inatakiwa kushinda mechi mbili tuu ili iweze kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia nchini Brazili.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja Bi.Failuna Mgata ambaye amekua mshindi wa mbio za kilometa 21 kwa wanawake wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.Kulia ni Mjane wa Marehemu Edward Sokoine.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimvalisha Medali mshindi wa kilometa tano wanaume wakati wa Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.Kushoto ni Rais wa Chama cha Riadha nchini Mhe.Antony Mtaka.

Katika hatua nyingine Mhe.Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kumuenzi Hayat Edward Moringe Sokoine kutokana na mchango wake wa kuletea Taifa maendeleo kwa kuhimiza wananchi kujituma, kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa mchezo wa riadha umeendelea kufanya vizuri kimataifa kwakua nchi imepata wawakilishi watakaoshiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2020 huko Tokyo Japan,mashindano ya riadha ya Dunia pamoja na Jumuiya ya Madola.

Mhe.Shonza ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Chama cha Riadha nchini inaendelea na maandalizi ya mashindano ya riadha ya kimataifa ya All Africa Games,World Championship na African Cross Country Championship ambayo Tanzania ndio itakuwa Mwenyeji.

“Mchezo huu wa riadha umeitangaza vyema nchi yetu kupitia wanariadha mbalimbali waliofanya vizuri kimataifa ambapo timu yetu ya Taifa ya mbio za nyika ilishiriki mashindano nchini Dernmark na kumaliza katika nafasi ya 8,10 na 11 kupitia wanariadha Failuna Matanga,Emmanuel Ginik,Gabriel Geay na Aliphonce Simbu”.alisema Mhe.Shonza.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali,Familia ya hayati Edward Sokoine pamoja kamati ya maandalizi ya Mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial Marathon yaliyofanyika Aprili 06,2019 Jijini Arusha yaliyokuwa na lengo la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alifariki miaka 35 iliyopita.

Hata hivyo  Rais wa Chama cha Riadha nchini Mhe.Antony Mtaka amewataka waandaaji wa mbio mbalimbali nchini kuzingatia Sheria na taratibu hususan usajili  wa mbio hizo katika  Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kabla ya kuzitangaza ama kuhamasisha wadau na wananchi kushiriki.

Naye mshindi wa mbio za Kilometa 21 kwa wanawake Bibi Failuna Matanga amesema kuwa mafaniko anayopata kupitia riadha ni kutokana na kujituma kufanya mazoezi pamoja na nidhamu katika mchezo huo.

Mbio hizo za Soikone Memorial Marathon zilishirikisha mbio za Kilometa 2 na nusu,Kilometa 05  na kilometa 21 ambapo Watoto,wasichana na wavulana walishiriki na washindi kupewa zawadi ikwemo pesa pamoja na medali.

67 thoughts on “Waziri Mkuu asisitiza Michezo ni Ajira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama