Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Akutana na Mtoto Aliyeshinda Tuzo Uingereza

Samuel Mwanyika (19) akiwa ameshika Tuzo wakati anatambulishwa kwa Wabunge Mjini Dodoma. Samuel alishinda Tuzo ya Stephen Thomas Iliyotolewa Na Taasisi ya Kimataifa ya watu wenye mtindio wa ubongo ya Uingereza baada ya kutuma picha ya Pundamilia wawili wakiota jua kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. watoto kutoka nchi 18 walishiriki shindano la picha kwa Mwaka 2017. (Picha na: Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa Tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya watu wenye mtindio wa ubongo (Down’s Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Wa kwanza Kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda Tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samuel Mwanyika, mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya kimataifa ya watu wenye mtindio wa ubongo (Down’s Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Katikati ni mama wa mtoto huyo Sophie Mshangama.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel Mwanyika aliyeshinda Tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa Juni 8, 2017 na Taasisi ya Kimataifa ya Watu Wenye Mtindio wa ubongo (Down’s Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Katikati ni mama ma mtoto huyo..

94 thoughts on “Waziri Mkuu Akutana na Mtoto Aliyeshinda Tuzo Uingereza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama