Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mhagama Afanya Ziara Mkoani Tanga Kukagua Hali ya Maandalizi ya Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Zena Said.

Na: Mwandishi Wetu:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amefanya ziara ya ukaguzi na kikao cha ndani pamoja na Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Tanga ili kupokea taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Mkoa wa Tanga utaadhimisha kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, sambamba na maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo yatafunguliwa rasmi tarehe 8 Oktoba, 2018 na Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Baba Askofu Anthoni Banzi wa Kanisa Katoliki la Mt. Anthon Jimboni Tanga, mahali ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa itafanyika tarehe Oktoba 14, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Bw. Henry Shekifu walipowasili uwanja wa Ramol Masiwani kuona maandalizi ya Vijana wa Halaiki.

Waziri Mhagama amesema Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu yatakuwa ya kihistoria hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuuenzi Mwenge wa Uhuru na kutafakari ukombozi na historia ya taifa kwa kuwasihi washiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo.

“Tumekuwa tukiwakumbusha wananchi kuendeleza falsafa ya Baba wa Taifa kupitia Mwenge wa Uhuru katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa na amani, utulivu na umoja.” Alisema Mhagama.

Aidha, Mhe. Mhagama alitoa wito kwa vijana kujifunza mazuri aliyoyafanya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere ili waweze kujitathimini na wakayatumie maonesho ya wiki ya vijana kuonesha kazi wanazojishughulisha nazo katika kuleta maendeleo ya taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana wa Halaiki alipowatembelea katika uwanja wa Ramol Masiwani kukagua Maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Vijana wa Halaiki wa Mkoa wa Tanga wakitoa heshima mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea kukagua Maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Tanga alipotembelea Uwanja wa Tangamano kukagua sampuli ya mabanda yatakayotumiwa na vijana katika maonesho ya wiki ya vijana yatakayofunguliwa rasmi tarehe 8 Oktoba, 2018.(Picha Zote na: Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Na Wenye Ulemavu)

Akiwa Mkoani Tanga Waziri Mhagama alitembelea na kuona Kanisa la Mtakatifu Anthon la Jimbo Katoliki la Tanga, ambapo ibada ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere itafanyika. Vilevile Uwanja wa Tangamano utakaotumika katika maonesho ya wiki ya vijana.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela alishukuru Mkoa wa Tanga kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu na kuahidi kumalizia maandalizi yote ya muhimu kwa wakati na muda waliopangiwa.

128 thoughts on “Waziri Mhagama Afanya Ziara Mkoani Tanga Kukagua Hali ya Maandalizi ya Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama