Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Lukuvi Akesha Akishughulikia Migogoro ya Ardhi

Baadhi ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi mida ya saa 9 usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.

Picha/Habari na: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza  majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.

Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

Mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam Bibi Fatuma Shami akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake kuvamiwa na kupata miliki pandikizi.

Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani Bibi Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro.

Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi.

Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

18 thoughts on “Waziri Lukuvi Akesha Akishughulikia Migogoro ya Ardhi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama