Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha ya Kiswahili

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya ardhi na Nyumba ya wilaya kutumia lugha ya Kiswahili katika kuandika hukumu.

Lukuvi alitoa maagizo hayo tarehe 5 Februari 2021 jijini Dodoma alipozungumza na Wenyeviti pamoja na Wasajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa nchi nzima kupitia Video (Video conference).

“Nasisitiza Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya mtumie lugha ya Kiswahili wakati wa kuandika hukumu zenu kama alivyoagiza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na nitashangaa kumuona mwenyekiti akiandika hukumu kwa lugha ya kiswahili’’ alisema Lukuvi

2 thoughts on “Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha ya Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama