Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Kairuki Akutana na Balozi wa Japan Nchini

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) ofisini kwake mjini Dodoma mapema leo tarehe 09 Mei, 2018.

Na. Samwel Mtuwa – Dodoma.

Waziri wa Madini,  Angellah Kairuki leo amekutana na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mjini  Dodoma lengo likiwa ni kujadiliana namna ya kushirikiana kwenye uwekezaji wa madini nchini.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili maandalizi ya Jukwaa la Uwekezaji  katika Sekta ya Madini kati ya  Tanzania na  Japan.

Alisema kupitia jukwa hilo, wadau kutoka nchi zote mbili watafahamu fursa za uwekezaji  katika sekta ya madini kama vile uongezaji  thamani ya madini yapatikanayo nchini na namna ya kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akiagana na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Japan mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

 

Kairuki aliongeza kuwa mbali na fursa mbalimbali katika sekta ya madini jukwaa hilo litaangalia namna ya kuongeza ajira kwenye sekta hiyo kwa kuwajengea uwezo wadau wa madini nchini.

Balozi Yoshida aliambatana na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya uwekezaji katika sekta  ya madini.

 

84 thoughts on “Waziri Kairuki Akutana na Balozi wa Japan Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama