Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Jafo Aziagiza Halmashauri Zote Nchini Kutenga Maeneo ya Michezo

Na Shamimu Nyaki – WHUSM


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo ametoa agizo kwa Halmashauri zote  nchini kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za michezo, huku akiagiza Wakurugenzi katika halmashauri hizo kusimamia vyema miundombinu ya michezo na kuhakikisha maeneo ya michezo hayavamiwi.


Mhe. Jafo ameyasema hayo leo Februari 08, 2021 jijini Dodoma katika kikao kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kilichoandaliwa na Wizara ya Habari ambacho kilijadili namna ya kuboresha Michezo katika shule za msingi na Sekondari.

7 thoughts on “Waziri Jafo Aziagiza Halmashauri Zote Nchini Kutenga Maeneo ya Michezo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama