Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Dkt. Mpango Aridhishwa na Maendeleo Ujenzi Jengo la NBS

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambao umekamilika kwa asilimia 82 hadi sasa na unatarjiwa kukamilika ifikapo Januari 2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa ( kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kuhusu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo mjini Dodoma mapema leo.

Mdhibiti wa Viwango katika mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mjini Dodoma Bw. Abdulkarim Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa mifumo mbalimbali inayofungwa katika jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati wa ziara yake katika mradi huo mjini Dodoma mapema leo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na Mkandarasi na wasimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu unaoendelea mjini Dodioma ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na mmoja wa mafundi wakati wa ziara yake leo mjini Dodoma kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu .

(Picha  zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

28 thoughts on “Waziri Dkt. Mpango Aridhishwa na Maendeleo Ujenzi Jengo la NBS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama