Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Bitek­­­­­­­o Ateta na Wenye Nia ya Kuwekeza Nchini

Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.

Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.

 

 

27 thoughts on “Waziri Bitek­­­­­­­o Ateta na Wenye Nia ya Kuwekeza Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama