Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Aagiza Kila Halmashauri Kuandaa Hati za Ardhi Zisizopungua Mia Kila Mwezi

Na Munir Shemweta, SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Ardhi. Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ametoa agizo kwa kila halmashauri nchini kutoa hati zisizopungua mia moja kwa kila mwezi.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika Mkoa wa Rukwa tarehe 19 Julai 2021 akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi sekta ya ardhi nchini, Dkt. Mabula alisema halmashauri kupitia idara zao za ardhi zinatakiwa kuandaa hati zisizopungua mia moja kwa mwezi katika yale maeneo ambayo viwanja vyake vimepimwa.

‘’kule ambako viwanja havijapimwa watendaji wake wanaweza kueleweka lakini mtu ana viwanja mia moja halafu anashindwa hati za idadi hiyo na wakati mwingine anatoa hati kumi tu huku akiwa amejiwekea lengo la kutoa hati mia moja’’ alisema Naibu Waziri wa Ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama