Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mkoani Manyara

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Katibu huyo yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu katika mkoa huo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo mbele ya mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa (katikati) mara baada ya kuwasilia katika Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Mama Fissoo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu. Kutoa kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage na Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa wa Mkoa Kennedy Kaganda.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akizungumza jambo alipokutana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) leo Ofisini kwake mjini Babati, Mkoani Manyara. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akisoma kwa makini nakala za Sheria ya Filamu na Kanuni zake mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) Ofisini kwake leo mjini Babati. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.

Kutoka Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa WA Mkoa wa Manyara Kennedy Kaganda na Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage wakifuatilia mazungumzo baina ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa (hawapo pichani) walipokutana ofisi kwa RAS –Manyara, mjini Babati leo. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Babati)

115 thoughts on “Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mkoani Manyara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama