Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi Wa Umma Wanaostahili Kulipwa Madai Ya Malimbikizo Ya Mishahara Baada Ya Uhakiki

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


TAARIFA KWA UMMA

TANGAZO LA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA BAADA YA UHAKIKI

 Wizara ya Fedha na Mipango Inapenda kuwajulisha Watumishi wa Umma kuwa, kikosi kazi kimemaliza uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara, zoezi hilo lilikamilika tarehe 5 Februari, 2018. Baada ya zoezi la uhakiki wa Watumishi wa Umma kukamilika, Serikali imejipanga kuanza kulipa madai sahihi kupitia kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa mkupuo mwezi Februari, 2018.

Aidha, Wizara ya Fedha na Mipango inawatangazia Watumishi wa Umma waliokuwa na madai hayo kuwa orodha ya majina ya wanaostahili kulipwa kutokana na Uhakiki huo kukamilika yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango ambayo ni www.mof.go.tz na Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo www.maelezo.go.tz

Imetolewa na;

KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

10 Februari, 2018

One thought on “Watumishi Wa Umma Wanaostahili Kulipwa Madai Ya Malimbikizo Ya Mishahara Baada Ya Uhakiki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama