Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi Wa Umma 27,389 Kulipwa Madeni Yao Mwezi Huu

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO,DODOMA

Serikali imesema baada ya kumaliza kufanya uhakiki wa madeni ya watumishi wa umma italipa madeni hayo katika mshahara wa mwezi februari 2018.

Akiongea na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema madai hayo yanajumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishwa mishahara.

“Kufikia tarehe 01 Julai, 2017 Serikali ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi Bilioni 127.6 kwa watumishi 82,111 wakiwamo walimu 53,925 waliokuwa wakidai Shilingi Bilioni 53.94 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote na wasiokuwa walimu 28186 wanaliokuwa wakidai Bilioni 73.6 sawa na asilimia 57.73”  Alisisitiza  Dkt. Mpango.

Akizungumzia matokeo ya uhakiki wa madeni hayo Dkt. Mpango amesema kuwa madai ya watumishi 27,389 kati ya 82,111 yenye jumla ya shilingi bilioni 43.39 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127.6 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa  bila marekebisho.

Waziri Dkt. Mpango aliongeza kuwa madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu 11,470.

akifafanua kuhusu matokeo ya madai hayo yamewezesha Serikali kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo.

Aidha, Waziri Dkt. Mpango amesema kuwa hatua hiyo ni matokeo ya juhudi za Serikali ambazo ni pamoja na  kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara watumishi hewa, vyeti feki na wasio na sifa.

Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.

170 thoughts on “Watumishi Wa Umma 27,389 Kulipwa Madeni Yao Mwezi Huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama