Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Watumishi Tume ya Utumishi wa Walimu Wapigwa Msasa Matumizi ya TEHAMA.

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel akiwasilisha mada kuhusu matumizi bora ya TEHAMA na vifaa vyake kwa watumishi wa Tume hiyo Manispaa ya Dodoma mapema leo kabla ya kuwaunganisha katika mfumo rasmi wa mawasiliano ya Serikali kwa njia ya mtandao.

Afisa Utumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Manispaa ya Dodoma Bw. Jastin Lwilla akimuonesha Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Tume hiyo Bi Devotha Gabriel sehemu ya vifaa vya TEHAMA vinavyotumika katika ofisi hiyo katika kutoa huduma.

Kaimu Katibu wa Tume hiyo Manispaa ya Dodoma Bi Leticia Mwakasitu (kushoto) akifuatilia mada kuhusu matumizi sahihi ya TEHAMA iliyowasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel, kulia ni Afisa utumishi wa Tume hiyo Manispaa ya Dodoma Bw. Jastin Lwilla.

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Tume hiyo Manispaa ya Dodoma mapema leo wakati wa ziara yake. (Picha zote na Frank Mvungi- Dodoma)

 

77 thoughts on “Watumishi Tume ya Utumishi wa Walimu Wapigwa Msasa Matumizi ya TEHAMA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama