Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wataalam wa Udhibiti Ubora wa Dawa Afrika Mashariki Wakutana Jijini Dar

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza alipokuwa akifungua kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayepia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Udhibiti Dawa Afrika Mashariki Hiiti Sillo akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam toka taasisi hizo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akifuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Dkt. Hiiti Sillo (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mdhibiti wa Dawa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wizara ya Afya nchini Rwanda Alex Gisagara na Kamishna wa Huduma za Famasi toka Uganda Seru Morries.

Afisa Msajili wa Dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Dk. Shani Maboko akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)

One thought on “Wataalam wa Udhibiti Ubora wa Dawa Afrika Mashariki Wakutana Jijini Dar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama