Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wasanii Nchini Waaswa Kuenzi Busara za Wazee

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bi. Joyce Fissoo akizungumza alipokuwa ameambatana na Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wajumbe wa kamati ya tamasha la muziki na sanaa za maonesho jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea nchini na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika.

Na: Mwandishi Wetu

Wasanii wa filamu nchi washauri kuheshimu na kutahmini mawazo na busara za wazee pindi wanapopata wasaa wa kukutana nao.

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alipokaribishwa kutoa neno wakati wa tukio fupi la Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherryl ‘‘Monalisa” kutoa shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania.

Fissoo alisema kuwa imekuwa ni desturi kwa baadhi ya vijana kuchukulia ushauri au mawazo yanayotolewa na wazee au watu wa makamu kuwa umepitwa na wakati hivyo hautakuwa na manufaa kwao.

Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa kamati ya tamasha la muziki na sanaa za maonesho jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania, Faza Lusozi Paul na kulia ni mama mzazi wa Monalisa, Bibi. Suzan Lewis.

Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania, Faza Lusozi Paul akizungumza jambo mara baada ya Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa (wapili kulia) kutoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Wakwanza kulia ni mama mzai wa Monalisa, Bibi. Suzan Lewis.

“Nikuombe mwanangu Monalisa nenda ukawe balozi mwema, waanbie wenzako waenzi na kuheshimu busara za wazee, naamini kwa kufanya hivyo mtayaona mafanikio ya kazi zenu,”

Aidha mama Fissoo ameongeza kuwa Monalisa amekuwa msanii wa mfano wa kuigwa hasa katika nyanja ya maadili kitu ambacho wasanii wengi wanapaswa kuzingatia .

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za dansi nchini, Mzee King Kikii akitoa nasaha kwa Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa (hayupo pichani) mara baada ya msanii huyo kutoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bi. Joyce Fissoo.

Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa (kushoto) akipongezwa na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho ambaye pia Bi. Asha Kabigili wakati masinii huyo alipofika katika kamati hiyo kwa ajili ya kutoa shukrani zake jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Wapili kutoka kushoto ni mama mzazi wa Monalisa, Bibi. Suzan Lewis na Mwanamuziki wa Vijana Jazz Band ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo Bi. Anna Waole.

Naye Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherryl ‘‘Monalisa” amesema kuwa anajisikia faraja kufika mbele ya watu ambao kwa namna moja ama nyingine walimtia moyo huku akiwa na ushindi ambao anaamini kuwa pamoja na juhudi zake binafsi maneno ya busara ya wazee hao yalimpa ari iliyosababisha kurejea akiwa mshindi.

“Nidhahiri kuwa maneno yenu ya busara ndiyo yametia chachu nikarejea nchini nikiwa mshindi wa Msanii Bora wa Kike Afrika, hivyo kwa kipekee sina budi kuwashukuru kwa duwa zenu na nitahakikisha naendelea kuenzi busara zenu,” alisema Monalisa.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi. Joyce Fissoo (waliokaa kushoto) na Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa(wanne kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.(Na: Mpiga Picha Wetu)

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Yvonne Cherry maarufu kwa jina la Monalisa ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika.

103 thoughts on “Wasanii Nchini Waaswa Kuenzi Busara za Wazee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama