Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wanzania 96 Wanufaika na Ufadhili wa Masomo Uholanzi

Na. Georgina Misama 

Watanzania 96 kutoka Serikalini, sekta binafsi na asasi za kiraia, wamenufaika na ufadhili wa masomo kutoka seriklai ya Uholanzi ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali hiyo kuchangia maendeleo nchini.

Akiongea katika ghafla fupi ya kuwaaga Watanzania hao, iliyofanyika jana katika ukumbi wa Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam, Balonzi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe.  Jaap Frederiks alisema kwamba Serikali ya Uholanzi kwa muda mrefu imekuwa ikichangia miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Balozi Jaap alieleza kuwa Watanzaia waliofaidika na mpango huo unaojulikana kama Netherlands Fellowship Programme – NFP, ni waajiriwa kutoka Serikalini, sekta binafsi, wafanyabiashara wadogo pamoja na waajiriwa kutoka Asasi za kirai.

“Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa moja kati ya wafaidika wakubwa wa ufadhili wa Masomo Nchini Uholanzi program inayojulikana kama “Netherlands Fellowship Programme – NFP” ambapo zaidi ya Watanzania 5000 wamefaidika na ufadhili huo katika kozi mbalimbali”. alisema Mhe. Balozi Jaap

Serikali ya Uholanzi imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo baadhi ya Watanzania pamoja na kuboresha Sekta ya rasilimali watu, tukiamini kwamba kupitia watu hao tunachangia katika maendeleo ya Taifa

Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi inchini humo.

Aidha, Naibu Balozi kutoka Ubalozi wa Ufalme wa Uholanzi Bibi Lianne Houben alisema kwamba ufadhili unaotolewa na Serikali ya Uholanzi kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje katika bajeti yake ya Ushirikiano wa maendeleo unagharamia gharama zote zitakazohitajika kipindi cha masomo.

Hafla ya kuwaaga Watanzania waliopata udhamini wa programu ya NFpiliongozwa na Mhe. Balozi wa Ufalme wa Uholanzi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, wawakilishi kutoka makampuni mbalimbali na Watanzania waliokwisha faidika na udhamini huo.

34 thoughts on “Wanzania 96 Wanufaika na Ufadhili wa Masomo Uholanzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama