Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wanariadha 8 Kuiwakilisha Tanzania Nchini Uingereza.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania (DSTV) Bw. Maharage Chande akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwakabidhi Bendera ya Taifa Wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Hawa ni baadhi ya Wanariadha wakiwa pamoja na Makocha wao ambapo jumla ya Wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika mbio nchini Uingereza ni nane (8) na wanatarajia kuanza safari yao hapo kesho 1 Agosti, 2017.

(Picha zote na Anitha Jonas)

502 thoughts on “Wanariadha 8 Kuiwakilisha Tanzania Nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama