Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wananchi wa Kijiji cha Melela Walipongeza Shirika la Pelum Tanzania.

1. Mmoja wa Wanufaika wa Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika kusimamia Sekta ya Kilimo (CEGO), Bi. Bahati Mwinyimvua mkazi wa Kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero (kushoto) akizungumzia kuhusu manufaa mbalimbali aliyoyoyapata kupitia mradi huo unaosimamiwa na Shirika la Pelum Tanzania na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID). Katikati ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Amini Membe na Afisa wa Pelum Tanzania, Jacquiline Massawe. Mafunzo hayo yanayotolewa na Pelum Tanzania na yalifanyika Septemba 16, 2017 Mkoani humo.

Na: Mwandishi Wetu

Wananchi wa Kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wamelipongeza Shirika la PELUM Tanzania kupitia Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika kusimamia Sekta ya Kilimo (CEGO) kwa kuwajengea uwezo Watendaji wa Serikali ya Kijiji na Wananchi kuweza kutatatua migogoro ya mipaka na mashamba katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa jana Mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Amini  Membe wakati wa semina ya mafunzo kwa Watendaji wa Serikali ya Kijiji na Wananchi kuhusu Mpango wa Matumizi ya Ardhi Vijijini.

2. Wananchi jamii ya Wafugaji wa Kijiji cha Mela, Wilaya ya Mvomero wakifuatiliaji mafunzo kutoka kwa na Shirika la Pelum Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika kusimamia Sekta ya Kilimo (CEGO). Mafunzo hayo yanayotolewa na Pelum Tanzania na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) yalifanyika Septemba 16, 2017 Mkoani humo.

Aliongeza kuwa kabla ya mradi wa CEGO, Ofisi yake ilikuwa ikipokea malalamiko ya kesi mbalimbali za migogoro ya ardhi, ambapo hata hivyo kwa sasa kesi hizo zimeelekezwa katika Mabaraza ya ardhi na kutoa fursa kwa Serikali ya Kijiji kujikita katika shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi.

Membe alisema semina na mafunzo mbalimbali yaliyotolewa na Shirika la PELUM Tanzania limesaidia wananchi wa kijiji hicho kufahamu taratibu na miongozo ya kisheria kuhusu hatua zinazopaswa kufuatwa katika mgawanyo wa matumizi ya ardhi baina ya jamii za Wakulima na Wafugaji.

“Katika eneo la kijiji chetu, kupitia PELUM Tanzania maeneo ya viwanja vingi sasa vimepimwa na wananchi wameelimika vya kutosha, kila mwananchi ataelewa eneo lipi linafaa kwa ajili ya matumizi ya makazi, malisho, kilimo na vyanzo vya maji, hivyo hakuna mwingiliano tena”  anasema Membe.

3. Mratibu wa Shirika la Pelum Tanzania, Donat Senzia akielezea kuhusu majukumu na kazi za shirika hilo, wakati wa mkutano baina yake na timu ya timu ya waandishi wa habari yaliyofanyika septemba 16, 2017 mkoani Morogoro.

Anaongeza kuwa kutokana na juhudi zilizoonyeshwa Na Kijiji hicho, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) umeweza kurasilimisha ardhi za wananchi wa kijiji hicho na kutoa Hati 360 kati ya Viwanja 760 vilivyopimwa.

“Kutokana na mipango na mikakati mizuri ikatika kijiji chetu, MKURABITA imeweza kusaidia kugharamia ujenzi wa Masijala ya Ardhi ya kijiji, ikiwemo kutupatia mabati, mbao, sementi na misumari na ujenzi wa masijala hiyo upo katika hatua za mwisho za kukamilika” anasema Membe.

Kwa upande Bi. Bahati Mwinyimvua anasema mradi wa CEGO umemwezesha kutambua nafasi na haki aliyonayo katika umiliki rasilimali ya ardhi, tofuati na dhana aliyoielewa hapo awali kuwa Mwanamke hapaswi kumuliki mali ikiwemo ardhi.

5. Afisa Tathimini na Ufuatiaji wa Shirika la Pelum Tanzania, Frank Maimo akielezea kuhusu majukumu na kazi za shirika hilo, wakati wa mkutano baina yake na timu ya timu ya waandishi wa habari yaliyofanyika septemba 16, 2017 mkoani Morogoro. (Na: Mpigapicha Wetu)

Anasema mafunzo ya mradi wa CEGO yamewawezesha kuondokana na utamaduni na mila za zamani za umiliki wa ardhi na badala yake kupata hati za kimila ambazo zitamwezesha mwananchi wa kawaida kuweza kupata mkopo katika taasisi za kifedha.

“Zamani sisi wanawake tulikuwa hatujui Sheria inatamka nini kuhusu haki ya kumiliki ardhi, lakini tunalishukuru Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa CEGO limetuwezesha kuweza kutambua nafasi na wajibu wetu katika umiliki wa rasilimali ardhi” anasema Bi. Mwinyimvua.

Mradi wa CEGO unaotekelezwa katika Halmashauri na Mikoa ya Iringa (Kilolo, Mufindi), Dodoma (Bahi, Kongwa), na Morogoro (Mvomero, Morogoro Vijijini) umeanza Disemba 2013 na unatarajia kukamilika Desemba 2017.

 

3 thoughts on “Wananchi wa Kijiji cha Melela Walipongeza Shirika la Pelum Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama