Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wanamichezo Watakiwa Kuzingatia Nidhamu

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimtambulisha mchezaji wa Serengeti Boys Zuberi Ada kwa mchezaji wa zamani wa timu ya Everton Bw.Leon Osman(mwenye T-shirt ya blue) walipokuwa wakiwasalimia wa katika wachezaji vijana wenye umri chini ya miaka 17 leo Jijini Dar es Salaam.

Na Lorietha Laurence

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wadau wa michezo nchini kuzingatia nidhamu na uvumilivu ili kufikia malengo ya klabu zao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia ujio wa klabu ya Everton nchini chini ya uratibu wa Kampuni ya SportPesa.

Katika mkutano huo, Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ujio wa uongozi wa timu ya Everton ni fursa kubwa kwa vilabu vya mpira wa miguu nchini katika  kujifunza mbinu mbalimbali za  kuendeleza na kukuza vipaji vya wachezaji wake.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Timu ya Everton Bw.Robert Elstone(katikati) na kulia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Everton Bw.Leon Osman leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Timu ya Everton Bw.Robert Elstone leo Jijini Dar es Salaam.

“Ujio huu ni muhimu na elimu tosha kwa vilabu vyetu nchini katika kuhakikisha vipaji vya wanamichezo vinakuzwa na kuendelezwa ili kufanikisha maendeleo ya sekta ya michezo “alisema Dkt.Mwakyembe.

Alisema mbali na elimu itakayopatikana kutoka kwa timu na uongozi wa Everton, ni fursa nzuri katika sekta ya Utalii kwa kuwa wageni hao wataweza kutembelea Mbuga za Wanyama,Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine mbalimbali vya kimichezo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na na wachezaji wa mpira wa miguu chini ya miaka 17 leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

Naye Mtendaji Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Everton Bw.Robert Elstone amesema kuwa lengo kuu la kuwepo Tanzania  ni kujenga uhusiano mzuri katika michezo husani mpira wa miguu kwa kuweka msingi mzuri wa kusaidia klabu za michezo na kukuza vipaji kwa vijana.

Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa Everton Bw.Leon Osman amesema kuwa ni muhimu kuendeleza vipaji vya vijana ili kuweza kupata wachezaji mahiri.

Kampuni ya SportPesa ambao ndio waratibu wa ziara ya Uongozi wa Everton nchini wameaahidi kuwepo kwa mechi ya kirafiki kati ya mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup na timu ya Everton Julai 13 mwaka huu katika Uwanja wa Mpira wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

75 thoughts on “Wanamichezo Watakiwa Kuzingatia Nidhamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama