Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wanafunzi 690 Wahitimu TEWW Katika Kipindi cha Mwaka 2017/2018

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Godfrey Mnubi akizungumza na wahitimu katika mafahali ya 54 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahitimu toka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo kwenye mahafali ya 54 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Naomi Katunzi akizungumza na wanajumuia wa TEWW katika mahafali ya 54 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na; Mwandishi Wetu

Imeelezwa kwamba katika mwaka wa masomo 2017/2018  jumla ya wanafunzi 690 wamehitimu katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambapo kati yao wahitimu 441 ni wa Stashahada na Wahitimu 249 ni wa Shahada.

Akizungumza wakati wa mahafali ya 54  ya Taasisi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara  ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amesema kuwa anaamini kuwa Wahitimu hao wameandaliwa vizuri na wameiva katika taaluma zao, hivyo watashiriki kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na bila shaka wataongeza nguvu ya kupambana na tatizo la kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taifa kwa ujumla inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kuwaandaa wataalamu wa ngazi mbalimbali katika fani za Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii pamoja na majukumu mengine mliyokabidhiwa”. Alisisitiza Dkt. Akwilapo.

Akifafanua amesema kuwa Wahitimu wa ngazi ya Shahada wanatarajiwa kuwa Wasimamizi, Walimu na Waratibu wa Elimu ya Watu Wazima ngazi za Mkoa na Wilaya, pamoja na kufanya tafiti zinazohusiana na Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii.

 Pia alibainisha  kuwa, Wahitimu wa ngazi ya Stashahada wanaandaliwa kuwa Walimu, Waratibu na Wasimamizi wa madarasa ya Kisomo; na wahitimu wa ngazi ya Astashahada wanaandaliwa kuwa Walimu wa madarasa ya Kisomo.

Ni dhahiri kuwa wataalamu walio hitimu leo wataenda kufanya kazi kwa ueledi zaidi ili kusaidia jitihada za serikali za kupambana na adui ujinga na hivyo kulifikisha taifa katika uchumi wa kati wa viwanda.

Napenda pia kusisitiza kuwa, kama ambavyo wengi wetu tunajua, mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano unaweka mkazo mkuu upo kwenye ujenzi wa Tanzania ya viwanda, Ili haya yote yafanyike ni lazima tuwe na watu wenye ujuzi na stadi mbalimbali.

“  Taasisi hii ni mdau muhimu katika kulifikia lengo kuwa na uchumi wa viwanda kwani inashiriki  kuandaa walimu, lakini pia vijana kupitia miradi na mipango mbalimbali iliyotajwa na Kaimu Mkurugenzi, Nasisitiza endeleeni kubuni njia nyingi za kuwapatia mafunzo Watanzania na hasa vijana ili waweze kushiriki kikamilifu katika Tanzania ya viwanda”. Alisisitiza Dkt. Akwilapo

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na wahitimu katika mahafali yaliyofanyika katika viwanja vya TEWW jijini Dar es Salaam.

Pia Dkt. Akwilapo alipongeza ushirikiano uliopo kati ya Taasisi na Asasi na Mashirika  ya Kimataifa kwani misaada yao ya kifedha, ushauri na mafunzo vimeisaidia Taasisi katika kutekeleza majukumu yake mbalimbali.

Aidha; aliihakikishia Taasisi hiyo  kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanyika ili kuendelea kutekeleza jukumu la kutoa elimu kwa ufanisi zaidi.

Naye    Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Naomi Katunzi amebainisha kuwa Taasisi hiyo imeweza kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu na mafunzo hasa katika fani Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya jamii kwa wahitaji walioko makazini, ambao sasa wanajiendeleza kitaaluma kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa.

“Upanuzi huu wa utoaji wa mafunzo hasa katika ngazi ya stashahada kwa njia ya Masafa umesaidia kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 4,524 katika mwaka wa masomo 2017/2018 na kufikia wanafunzi 5815 mwaka wa masomo 2018/2019.” Alisisitiza Dkt. Katunzi

Alibainisha kuwa ongezeko hili ni sawa na asilimia 77.8%. Aidha, ongezeko hili limechangia pia kuongeza mapato ya ndani ya taasisi na kuweza kuboresha baadhi ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na kugharamia uendeshaji wa madarasa ya kisomo nchini kama alivyoeleza Mkurugenzi/Mkuu wa chuo.

“Ni imani yangu kuwa wahitimu hawa wataendelea kuwa chachu ya Maendeleo nchini hususan katika sekta ya Elimu ya Watu Wazima. Kwani kama tunavyofahamu, kwa sasa kuna changamoto za kutokukujua kusoma, kuandika na kuhesabu miongoni mwa vijana na Watu wazima nchini. Hivyo ni matarajio yangu wahitimu hawa watasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na changamoto ya kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu huko wanakokwenda “Alisisitiza Dkt. Katunzi

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt.  Godfrey Mnubi amesema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuhakikisha kuwa  inaendelea kuongeza fursa zaidi katika utoaji wa elimu, kwa kupanua wigo wa utoaji wa programu zake za elimu na mafunzo kwa kutumia njia ya Ujifunzaji Huria na Masafa kwa ngazi ya Stashahada kwa kuongeza vituo kutoka 33 hadi 42.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuwafikia walengwa wengi zaidi kujiunga na programu za mafunzo yanayotolewa na Taasisi hii huku wakiwa wanaendelea na 3 majukumu yao katika sehemu zao za kazi, na hivyo kuepuka upungufu wa nguvu

Mahafali haya ya 54 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kampasi ya Dar es Salaam yamewashirikisha wahitimu 690 katika ngazi mbalimbali ikiwemo shahada na stashahada.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama