Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wakufunzi Acheni Lugha Zinazowakatisha Tamaa Wanachuo

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Reli cha Tabora Eng. Richard Lauwo (kulia), wakati alipotembelea chuoni hapo jana katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mwalimu Queen Mlozi. (Picha na: Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

Na: Tiganya Vincent, RS-Tabora

WAKUFUNZI  wametakiwa kutumia lugha zinazosaidia wanachuo kujengeka kimaadili  badala ya kuwakatisha tamaa kwa maneno ambayo yanawavunja moyo wa kuendelea kujifunza na kubadili tabia zao endapo zinakuwa hazina tija  katika maendeleo yake ya kitaaluma.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbawara wakati wa ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo cha Reli kilichopo Tabora.

Mkuu wa Chuo cha Reli cha Tabora Eng. Richard Lauwo (kushoto), akifafanua jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipotembelea chuoni hapo.

Alisema kuwa lazima wakufunzi  watambue wapo pale kwa ajili ya wanachuo  kwani wasingekuwepo nao wasingekuwa na kazi ya kufanya.

Profesa Mbawara aliongeza kuwa Mkufunzi Mzuri ni yule anapoona maendeleo ya mwanachuo wake hayaridhishi ni jukumu lake la kukaa naye na kumsikiliza na kisha kumshauri njia nzuri ya kumuondoa pale alipo na kwenda mbele zaidi.

Aliwataka wanafunzi kuwa waadilifu na kusoma kwa bidii na kuongeza kuwa uadilifu uanzia katika shule na sio kazini.

Kwa upande wa Wanachuo hao waliomba Serikali iwasaidie kupatiwa mikopo na fedha za mafunzo kwa vitendo kama ambavyo wanafunzi  wa Vyuo vingine hapa nchini.

151 thoughts on “Wakufunzi Acheni Lugha Zinazowakatisha Tamaa Wanachuo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama