Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JKCI Watakiwa Kutumia Baraza Wafanyakazi

Na: Mwandishi wetu

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kulitumia Baraza la wafanyakazi kufikisha malalamiko yao na kutoa maoni ya utendaji kazi na siyo vinginevyo.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la JKCI.

Alisema  baraza hilo ni la  muhimu kwani ndilo linalotambulika kwa mujibu wa kisheria kama watalitumia  vema kufikisha malalamiko yao,  maoni na ushauri wa sheria na si kulitumia kama ‘forum’ (majukwaa) ambayo hayatambuliki kisheria litawasaidia kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na wafanyakazi.

“Nina imani  kubwa kwa uongozi wa taasisi hii kwamba utapokea malalamiko, ushauri na maoni ya wafanyakazi wake kupitia baraza hili na kuyafanyia kazi. Hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi hii katika kuhudumia wagonjwa,” Mwalwisi alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema kuzinduliwa kwa baraza hilo kunadhihirisha jinsi ambavyo taasisi hiyo imekua katika utoaji huduma.

“Kwa hiyo leo kwetu ni siku muhimu kwani baraza hili lililozinduliwa ni la muhimu litatusaidia katika kuimarisha utendaji kazi wa taasisi,” alisema.

Prof. Janabi aliwasisitiza wajumbe waliochaguliwa kuliongoza baraza hilo kuwa chachu katika kutimiza wajibu wao kuisaidia taasisi kuendelea kutimiza dhima yake ya kutoa huduma bora za kimatibabu na za kitafiti ili iweze kufikia lengo iliyojiwekea la kuwa kituo bora cha kutoa huduma za afya ya moyo Afrika.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi hiyo Prof. William Mahalu aliupogeza uongozi wa Taasisi kwa kusimamia na kuhakikisha Baraza la wafanyakazi linaundwa na kuanza kufanya kazi zake kwa wakati.

Prof. Mahalu alisema tangu  kuanzishwa kwa Taasisi hiyo huu ni mwaka mmoja na nusu wameweza  kuwa na baraza la wafanyakazi jambo ambalo siyo rahisi kwani wengine wanakaa hadi miaka mitatu  wakibisahana nani awe Katibu wa kuliongoza baraza lao.

 

 

72 thoughts on “JKCI Watakiwa Kutumia Baraza Wafanyakazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama