Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wajasiriamali Korogwe Kuandaliwa Eneo la Uzalishaji

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Kissa Gwakisa akifungua semina ya wajasiriamali juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya wajasiriamali linaanza kufanyiwa maandalizi ya awali ili kuondoa changamoto ya eneo la kuzalisha kwa mjasiriamali mdogo.

Alitoa maagizo hayo wakati akifungua mafunzo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wajasiriamali wadogo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambapo wajasiriamali 104 walihudhuria.

Gwakisa alisema eneo la uzalishaji ni kilio cha wazalishaji wadogo wengi na hivyo hatua hiyo itawasaidia wajasiriamali hao kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha.

Kwa upande wake, Afisa masoko mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka, alitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwajali wajasiriamali hao kwani itawasaidia kupata leseni ya kutumia alama ya ubora na vilevile huduma hiyo kwa mjasiriamali mdogo ni bure.

Afisa Masoko mwandamizi Bi. Gladness Kaseka (TBS) akitoa elimu ya Viwango kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere wilayani Korogwe.

Kaseka aliwakumbusha kuomba mafunzo maalum TBS, ambapo TBS hufanya kushirikiana na SIDO na TFDA bila gharama yoyote.

Wajasiriamali waliopata elimu hiyo wamefurahishwa na Shirika hilo kuwafikia na kuwaongezea uelewa wa viwango na kuwajulisha juu ya fursa ya bure kwao kupata leseni ya TBS itakayowasaidia kuuza bidhaa zao popote na ushindani halali sokoni.

Sambamba na mafunzo hayo Shirika pia lilitoa elimu ya viwango kwa wananchi katika maeneo ya stendi  ya zamani ya manundu, stendi mpya, soko la manundu na sabasaba, pamoja na  wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyerere yenye jumla ya wanafunzi na walimu 746.

Wajasiriamali wilayani Korogwe wakipata elimu juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS .

 

 

6 thoughts on “Wajasiriamali Korogwe Kuandaliwa Eneo la Uzalishaji

 • August 10, 2020 at 9:49 am
  Permalink

  My family all the time say that I am killing my time here at net,
  except I know I am getting knowledge everyday by reading such nice posts.

  Reply
 • August 24, 2020 at 7:42 pm
  Permalink

  It’s the best time to make some plans for the future and it is time to be happy.

  I have read this post and if I could I want to suggest you few
  interesting things or suggestions. Maybe you could write next articles referring to this article.
  I wish to read more things about it! 3gqLYTc cheap flights

  Reply
 • August 26, 2020 at 9:45 pm
  Permalink

  Do you mind if I quote a couple of your posts as long as I provide credit and sources back
  to your weblog? My blog is in the exact same niche as yours and my users would really benefit
  from some of the information you provide here. Please let
  me know if this alright with you. Thanks! 32hvAj4 cheap
  flights

  Reply
 • August 27, 2020 at 3:41 am
  Permalink

  Great post! We are linking to this particularly great article on our website.
  Keep up the great writing.

  Reply
 • August 31, 2020 at 5:23 am
  Permalink

  I’m gone to convey my little brother, that he should also visit this webpage on regular
  basis to obtain updated from newest information.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama