Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida Waendelea Kunolewa Namna ya Kutumia Mfumo Mpya wa Malipo Epicor 10.2.

Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo huo kwa Wahasibu wa Manispaa ya Singida, leo Jijini Dodoma.

 

Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akiwaelekeza Wahasibu wa Halmashauri ya Iramba maeneo yaliyoboreshwa katika mfumo huo mpya wa malipo, leo Jijini Dodoma.Watumishi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sector za Umma (Ps3) Bw. Majiga Robert (wa kushoto) na Jimmy Mungai (wa kulia) wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2  yaliyoandaliwa na TAMISEMI  kwa kushirikiana na PS3, leo Jijini Dodoma

Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida wakijengewa uwezo namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo ulioboresha (Epicor 10.2) unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote  za Serika za Mitaa hapa nchini

Afisa Msimamizi Fedha Mkoa wa Dodoma, Bw. Elisius Gujenji (aliyesimama) akiwaelekeza jambo juu ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) Wahasibu wa Halmashauri ya Chamwino, leo Jijini Dodoma.

(Picha Na; Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.)

41 thoughts on “Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida Waendelea Kunolewa Namna ya Kutumia Mfumo Mpya wa Malipo Epicor 10.2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama