Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wafanyakazi wa JKCI Wapewa Mafunzo na Kampuni ya Medtronic ya Mfumo wa Umeme wa Moyo

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (pace maker) ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.

Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG) kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.

Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Medtronic ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG) kwa wafanyakazi wa JKCI yaliyoandaliwa na kampuni hiyo.

Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG) unavyofanya kazi mwilini wakati wa mafunzo hayo yanayoenda sambamba na vitendo ya siku tano yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Ahmed Osman (hayupo pichani) kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG) unavyofanya kazi mwilini. (Picha na JKCI)

182 thoughts on “Wafanyakazi wa JKCI Wapewa Mafunzo na Kampuni ya Medtronic ya Mfumo wa Umeme wa Moyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama