Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wafanyabiashara Urambo Wanufaika na Mpango wa Urasimishaji

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akizungumza na wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabaro jana. Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Kamati hiyo wapo kkatika ziara ya makabidhiano ya uongozi kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga na Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akizungumza na wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabaro jana. Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Kamati hiyo wapo kkatika ziara ya makabidhiano ya uongozi kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga na Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe.

Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Angelina Kwinga akizungumza wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani wilayani humo na Kamati ya Uongozi ya MKURABITA chini ya Mwenyekiti wake Balozi Daniel Ole Njolay (katikati) jana wilayani Urambo. Kulia ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe.

Mwenyekiti wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati akisisitiza jambo wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabora na Kamati ya Uongozi ya MKURABITA chini ya Mwenyekiti wake Balozi Daniel Ole Njolay (hayupo pichani) jana wilayani Urambo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Angelina Kwinga na Makamu Mwenyekiti mpya wa MKURABITA Bibi. Imaculate Senje (Kushoto).

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bibi. Seraphia Mgembe akisisitiza jambo wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabora na Kamati ya Uongozi ya MKURABITA chini ya Mwenyekiti wake Balozi Daniel Ole Njolay (kushoto) jana wilayani Urambo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Margreth Nakainga.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Margreth Nakainga akisisitiza jambo wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabora na Kamati ya Uongozi ya MKURABITA chini ya Mwenyekiti wake Balozi Daniel Ole Njolay (wa pili kushoto) jana wilayani Urambo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Angelina Kwinga na Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe.

Makamu Mwenyekiti wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) aliyemaliza muda wake Profesa Ado Lupala akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabora na Kamati ya Uongozi ya MKURABITA chini ya Mwenyekiti wake Balozi Daniel Ole Njolay (kulia) jana wilayani Urambo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Angelina Kwinga , Mwenyekiti maliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati na Makamu Mwenyekiti mpya Bibi. Imaculate Senje.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga wakipitia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji katika Halmashauri ya wilaya ya Urambo wakati wa kikao baina ya wafanyabiashara wanufaika wa Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) wilayani Urambo mkoani Tabaro jana. Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Kamati hiyo wapo katika ziara ya makabidhiano ya uongozi kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akielezea jambo alipotembelea Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji Biashara wilayani Urambo mkoani Tabora jana. Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Kamati hiyo wapo katika ziara ya makabidhiano ya uongozi kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa MKURABITA aliyemaliza muda wake Profesa Ado Lupala, Makmau Mwenyekiti mpya Bibi. Irene Senje, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo Bibi. Margreth Nakainga na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Isack Nkeyemba. Kituo hicho cha pamoja kimewezeshwa na MKURABITA kwa lengo la kuwarahisishia wananchi kurasimisha biashara zao kupitia usajili.

Muonekano wa Jengo linalotumika kama Ofisi za Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji Biashara katika Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora. Kituo hicho kimewezeshwa chini ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa lengo la kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma za usajili wa biashara zao kwa kuwaweka wahusika wote wa usajili (TRA, Brella, Afisa Biashara na Taasisi za Kifedha) katika jengo moja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (kushoto) akiangaia jinsi mashine ya kukamua mafuta ya Alizeti inavyofanyakazi walipomtembelea mmoja ya wanufaika wa MKURABITA wilayani Urambo mkoani Tabora jana. Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Kamati hiyo wapo katika ziara ya makabidhiano ya uongozi kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Margreth Nakainga, mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Bibi. Anna Mwasha, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati na Mreatibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (wa tatu kulia) na wajumbe wa Kamati yake wakikagua bustani ya mmoja wa wananchi wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora aliyenufaika na MKURABITA Bw. Gilbert Kihumo (wa pili kulia) jana wilayani humo. Mwenyekiti huyo na wajumbe wake wapo katika ziara ya makabidhiano ya uongozi na majukumu kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe, Mtaalamu Mshauri toka Kampuni ya GODTEC, Makamu Mwenyekiti wa MKURABITA, Bibi. Irene Senje na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Bibi. Margreth Nakainga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Kampuni ya Urambo Wazalendo na wajumbe wa Kamati yake mara baada ya kupokea taarifa yao jana wilayani Urambo. Mwenyekiti huyo na wajumbe wake wapo katika ziara ya makabidhiano ya uongozi na majukumu kutoka kwa Kamati iliyomaliza muda wake mapema hivi karibuni. Kampuni hiyo imeanzishwa na baadhi ya wanufaika wa MKURABITA wilayani Urambo kupitia elimu waliyopewa na MKURABITA kwa kushirikiana na Kampuni ya Kukuza Biashara ya GODTEC. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Urambo).

61 thoughts on “Wafanyabiashara Urambo Wanufaika na Mpango wa Urasimishaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama