Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wadau Usimamizi Kemikali Sekta ya Mafuta, Gesi Wakutana Dar Es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bi. Magdalena Mtenga, akifungua (kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira)) warsha ya wadau wa Usimamizi wa Kemikali na Kemikali Taka za Sekta ya Mafuta na Gesi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, Dar es Salaam .

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na washiriki wa warsha kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa ufunguzi wa Warsha ya Usimamizi na Usimamizi wa Kemikali taka za sekta ya Mafuta na Gesi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Risper Koyi (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa wadau kuhusiana na Mikataba ya Kimataifa ya Usimamizi wa Kemikali.

Wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka katika Sekta ya Mafuta na Gesi kutoka Taasisi za Umma na Binafsi wakifuatilia mada katika warsha ya Usimamizi na Usimamizi wa Kemikali taka za sekta ya Mafuta na Gesi inaeyoendelea jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga (aliyekaa katikati) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto, waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam .

134 thoughts on “Wadau Usimamizi Kemikali Sekta ya Mafuta, Gesi Wakutana Dar Es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama