Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Jiepusheni na Rushwa-Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa mashine 10 za kufyatua matofali alizokabidhiwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kabla ya kufungua semina ya Bodi hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. Mashine hizo zitagawiwa bure kwa vikundi vinavyojishugulisha na ufyatuaji matofali. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na wanne kuil ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Joseph Nyamhanga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Locks and Systems Limited ya Dar es salaam, Linda Mwamukonda kuhusu vitasa, bawaba na milango ya kielektroniki wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye viwanja vya Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

Baadhi ya washiriki wa Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua semina hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ngao ya shukurani kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dkt. Ludigija Boniface Bulamile baada ya kufungua semina Endelevu ya 29 ya Bodi hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi walioshiriki katika Semina Endelevu ya 29 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi baada ya kufungua semina hiyo kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 18, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa, Makame Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi, Joseph Nyamhanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dkt. Ludigija Boniface Butamile.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

139 thoughts on “Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Jiepusheni na Rushwa-Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama