Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Viongozi wa Kimila Nchini Himizeni Uzalendo na Utaifa

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Amani Lukumay (Kulia) baada ya kuwasili katika Chuo cha Ufundi cha Arusha (Arusha Technical College) kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiongozana na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai kuelekea mahali ambapo mkutano wa kimila unafanyika.

Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai Bw. Isack Lekisongo (kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na Ukoo wa Mollel kuingia katika eneo ambalo hutumika kufanya mila mbalimbali za kabila hilo, eneo hilo limo ndani ya nyumba za Waalimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).

Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akijadiliana jambo na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai , alipohudhuria mkutano wa kimila wa viongozi hao leo Jijini Arusha.

Viongozi na Wazee Mbalimbali wa kabila la Kimasai wakimsikiliza Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika Picha) alipokuwa akizungumza nao wakati wa mkutano wa kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha. (Picha na Lorietha Laurence

Viongozi na Wazee Mbalimbali wa kabila la Kimasai wakimsikiliza Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika Picha) alipokuwa akizungumza nao wakati wa mkutano wa kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Aliyekaa) akipewa fimbo na Mwenyekiti Mstaafu wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai Bw. Langidare Manapi (kulia) ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika kabila hilo, kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi hao Leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisema jambo wakati wa Mkutano wa Kimila wa Viongozi na Wazee wa Kimasai leo Jijini Arusha, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddy Kimata ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kulia ni Mwenyekiti wa Wazee wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo.

202 thoughts on “Viongozi wa Kimila Nchini Himizeni Uzalendo na Utaifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama