Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Viongozi wa Kimila Kutoka Jamii ya Kimasai Tanzania Wamlilia Waziri Mwakyembe Kuhusu Eneo la Kufanyia Mikutano ya Kimila

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kimila kutoka jamii ya Kimasai nchini akiwa ameshikana mkono na Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu wa Kimasai Tanzania Chifu. Isack Meijo Ole Kisongo (wapili kulia) mara baada ya viongozi hao kuwasilisha malalamiko yao leo Jijini Dodoma kuhusu mgogoro wa eneo la kufanyia mikutano ya kimila lililoko Mjini Arusha kupunguzwa pamoja na jengo lao walilojengwa kusimamishwa ujenzi kwa zaidi ya miaka kumi hivyo kusababisha changamoto ya utekelezaji wa shughuli zao za kimila,wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Ukoo wa Laizer Tanzania Bw.Oltetiai Sozi,anayemfuata (wapili kushoto) ni Mwenyekiti wa Ukoo wa Mollel Tanzania Bw.Saitabau Mollel, kutoka kushoto wa kwanza ni Mwenyekiti wa Kamati ya Dira kwa Jamii ya Kimasai Tanzania Zablon Ole Muterian .

Mwenyekiti wa Kamati ya Dira kwa Jamii ya Kimasai Tanzania Bw. Zablon Ole Muterian (kulia) akimwonyesha Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ( baadhi ya nakala za barua,taarifa na picha zinazohusu mgogoro wa eneo lao la kufanyia mikutano ya kimila kwa jamii ya Kimasai nchini lililopo Arusha Mjini namna lilivyopunguzwa na zuio la kujenga ukumbi wao wa mikutano ulivyofanyika na kusababisha kero kwao wakati wa kufanya mikutano yao ya kimila kitaifa kwa kila mwezi katika kikao kilichoendeshwa na Mheshimiwa Waziri,wakiwemo viongozi wa Idara ya Utamaduni pamoja na wazee hao wa kimila kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Viongozi wa Kimila kutoka Jamii ya Kimasai Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza hatua atakazo chukua katika kufanikisha anatatua mgogoro wao kuhusu eneo lao la kufanyia shughuli za kimila lililopo Mjini Arusha, leo Jijini Dodoma mara baada ya wazee hao kumweleza changamoto wanazozipata katika kuendesha shughuli za za kimila tangu ya eneo hilo lilipopunguzwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama