Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vijana Group Waomba JPM Adhibiti Vijiwe Vya Pombe na Kamari

Mwakilishi wa kundi la Vijana Group Bw.Timotheo Umbayda akieleza jambo mbele ya Waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu utafiti kwa vijana pamoja na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano, leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari Idara ya Habari –MAELEZO Bw.Frank Shija .(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)

Na.Paschal Dotto

Muungano wa vijana kutoka Karatu mkoani Arusha maarufu kama Vijana Group wamemuomba Rais Mh.John Pombe Magufuli kudhibiti vijiwe vya Pombe na Kamari vinavyopotezea muda vijana ili wajikite katika shughuli za ujenzi wa wa taifa kama sera ya serikali ya wamu ya tano ya Tanzania ya viwanda inavyoelekeza.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam jana na Bw.Timotheo Umbayda alipozungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti kuhusu vijana na ujenzi wa taifa utafiti iliofanyika katika mikoa 8 ya Tanzania bara yakiwemo Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha huku utafiti huo ukijikita zaidi kuchukua maoni ya vijana juu ya utendaji kazi wa serikali ya Awamu ya tano pamoja na changamoto zinazowakabili vijana katika mikoa hiyo.

“Wakati umefika Mh.Rais aone namna ya kuwasaidia vijana wanaoshinda kwenye vijiwe vya Pombe, na wale wanaoshinda kwenye michezo ya kubahatisha na pool table, waondokane na tabia hizo na hatimaye wafanye kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla”,alisema Bw.Umbayda

Aidha Bw.Umbayda alisema kuwa katika utafiti wao wamebaini kuwa vijana wengi wa kitanzania hasa waishio mijini wamekuwa wakiutumia muda wao vibaya hususan kufanya maovu badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo na uzalishaji mali.

Alisema vijana ndio kioo cha jamii hivyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taifa linapata maendeleo, hivyo wakijielekeza katika kukaa vijiweni kusikokuwa na tina Tanzania haitaweza kupata maendeleo na itaendelea kuwa tegemezi wakati nguvukazi ya kutosha ipo na ina uwezo wa kufanya kazi.

Aliendelea kusema kuwa Rais Magufuli atoe maelekezo kwa vijana kupitia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya ya jinsi ya kuwasaidia vijana ili washiriki katika kujenga uchumi kwa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali, ufundi, ufugaji na ujasiriamali ili kuongeza nguvu katika ukuaji wa uchumi.

Bw. Umbayda alisema kuwa katika kuwajenga vijana kimaadili ni muhimu kwa taifa kuwashirikisha viongozi wa dini katika kuwaombea na kuwafundisha maadili kwani taifa lenye maadili ndiyo taifa lenye maendeleo.

Kikundi cha Vijana group kinaundwa na vijana watano wa kitanzania kutoka Karatu mkoani Arusha, ambao ni waalimu na lengo la kikundi chao ni kutumia taaluma yao ya ualimu kufundisha vijana jinsi ya kutumia vizuri muda na kujiletea maendeleo badala ya kukaa vijiweni.

Hivi karibuni vijana wengi hasa wa mijini wameingia kwenye wimbi la kukaa vijiweni bila kufanya kazi yoyote huku wakishiriki katika michezo ya kubahatisha maarufu kama ‘Kubeti’ badala ya kufanya kazi.

132 thoughts on “Vijana Group Waomba JPM Adhibiti Vijiwe Vya Pombe na Kamari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama