Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Usimamizi wa Rasilimali za Nchi Wampaisha Rais Magufuli

Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry Dkt. Charles Gadi (katikati) akifanya maombi maalum ya kuzuia mvua zisilete madhara kwa jamii mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchungaji James Mwageni na kulia ni Mchungaji Palemo Massawe.

Na: Frank Shija

Rais John Pombe Magufuli amezidi kupongezwa kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia rasilimali za Taifa ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na kufanya maombi ya kuzuia kunyesha kwa mvua zenye madhara.

“Napenda kuchukua nafasi hii kwa dhati kabisa kama kiongozi wa dini kumpongeza Rais Magufuli kwa kufanikiwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi yetu hususan eneo la madini ya dhahabu na vito,hadi kuwezesha kurejeshwa sehemu ya malimbikizo ya kodi ambayo huenda tusingeipata kama siyo jitihada zake”, alisema Askofu Gadi.

Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry Dkt. Charles Gadi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maombi maalum ya kuzuia mvua zisilete madhara kwa jamii mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchungaji James Mwageni na kulia ni Mchungaji Palemo Massawe. (Picha na: Eliphace Marwa)

Askofu Gadi amesema kuwa kama si ujasiri aliouonyesha Rais Magufuli katika kupigania raslimali za nchi, kama isingekuwa msimamo wake wa kutoyumbishwa na makampuni ya madini huenda makubaliano yasingefikiwa kama ilivyo sasa.

Awali akizungumza kabla ya kuanza kuomba kuhusu kuzuia mvua zenye madhara kunyesha kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wanyonge jambo linaloelezwa kuwa ni hatua nzuri kwa Serikali kuweka misingi yenye mikubwa na imara.

Askofu Gadi amesema kuwa wamekuwa na desturi ya kufanya maombi mbalimbali ya kuliombea Taifa kuepukana na majanga mbalimbali yakiwemo mafuriko, hivyo maombi haya maalum ya kuzuia mvua yamekuja wakati muafaka ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa wametoa tahadhari kuhusu uwepo wa mvua kubwa.

Aidha, Kiongozi huyo wa Kiroho amesema kuwa wameleta maombi hayo maalum ya kuzuia mvua zenye madhara kwa imani kwamba mvua za Mungu hazileti madhara mabaya kwa watu, kwani alishaapa baada ya gharika ya Nuhu kwamba hatakaa aiangamize dunia tena kwa maji.

72 thoughts on “Usimamizi wa Rasilimali za Nchi Wampaisha Rais Magufuli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama