Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ulinzi wa Kimtandao Kuimarishwa Nchini Ili Kulinda Mifumo

Na: Jonas Kamaleki

Serikali  kushirikiana na sekta binafsi wanaweza kujenga msingi wa kitaifa katika kuimarisha Usalama katika ulimwengu mzima kwa ujumla na kudondokana na uhalifu wa kimitandao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Matt Sutherland wakati wa ufunguzi wa Warsha ya masuala muhimu katika kuweka miondombinu ya kiusalama katika mitandao.

Sutherland amesema kuwa uhalifu wa kimitandao haungalii mipaka ya nchi bali unaweza kutokea mahali popote na wakati wowote. Alisisitiza hilo amesema kuwa mwezi Mei mwaka huu shambulio la kimtandao lilipiga mifumo karibu nchi 100 Duniani..

“Katika shambulio hilo, Uingereza tuliathirika sana hasa katika sekta ya Afya ambapo kompyuta katika Hospitali nyingi zilishindwa kufanya kazi na kusababisha madaktari kushindwa kupata taarifa za wagonjwa, ” alisema Sutherland .

Ameongeza kuwa Septemba mwaka jana wakati lilipotokea tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, Uingereza ilikuwa mstari wa mbele katika kurejesha miondombinu ya shule ya sekondari Ihungo kwani katika tukio hilo waliotharika zaidi ni wanafunzi.

Akiongelea suala la kiusalama, Naibu Balozi huyo amesema kuwa katika Mkutano wa Kilele utakaofanyika mwakani utangalia masuala mbalimbali ya kiusalama ikiwemo kupambana na ugaidi wa kimataifa,uhalifu wa makusudi, mashambulio ya kimtandao  utumwa mambo leo na vitisho vya demokrasia.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Warsha, Dkt. Martin Koyabe kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (CTO) amesema kuwa lento la Warsha hii ni kuwawezesha watumishi wa umma na wa sekta binafsi kufahamu miondombinu ya kiusalama katika sekta muhimu za kiuchumi ili kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Dkt Koyabe amesema kuwa warsha hii inakusanya watumishi pamoja ili kuwa uelewa wa kuainisha maeneo muhimu ya kiuchumi yanayotakiwa mifumo yake ya kimitandao kulindwa ili uchumi usiathirike endapo mifumo hiyo inashambuliwa.

“Serikali ni muhimu kutunga sera, sheria na kanuni za kuweka ulinzi wa kimitandao ili tusiathirike wakati shambulio linapotokea,” alisema Dkt. Koyabe

Ameongeza kuwa zipo changamoto kadhaa katika kutekeleza programu za ulinzi wa kimitandao. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa bajeti, uhaba wa wataalaam na utaalaam katika eneo la ulinzi wa kimitandao.

Warsha hii ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na CTO katika kukamilisha Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Kimitandao (National Cyber Security Strategy).

29 thoughts on “Ulinzi wa Kimtandao Kuimarishwa Nchini Ili Kulinda Mifumo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama