Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ujumbe Kutoka Kwa Mfalme wa Oman Wawasili Jijini DarLeo

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akimpokea Waziri wa Mafuta na Gesi toka Oman Dkt. Mohamed Hamed Al- Rumhi ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili na meli ya mfalme ya Fulk Al Salamah katika bandari ya Dar es Salaam leo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni Mfanyabiashara wa Tanzania Seif A. Seif.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo.

Meli ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah ikiwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu takribani 350 kutoka Oman.

Meli ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah ujumbe wa watu takribani 350 kutoka kwa mfalme wa Oman ikitia nanga katika bandari ya Dar es Salaam leo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi akiwa na kiongozi wa ujumbe kutoka Oman Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohammed Hamed Al-Rumhi wakitazama ngoma toka kwa moja ya kikundi cha watumbuizaji mara baada ya meli ya Fulk Al Salamah ikiwa na ujumbe wa watu 350 kutoka kwa mfalme wa Oman kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam leo. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

8 thoughts on “Ujumbe Kutoka Kwa Mfalme wa Oman Wawasili Jijini DarLeo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama