Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ufunguzi wa Maonesho ya Utalii Zanzibar Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonesho ya Utalii Zanzibar, katikati Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, wakielekea katika mabanda ya maonesho baada ya kuwasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwakilishi wa Kikundi cha JULUKIZA Ndg. Ali Bakari akitowa maelezo ya vitu vya mbalimbali vya Asili wakati akitembelea Maonesho ya Utalii yaliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Habari na Uhusiano wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Ndg. Amour Mtumwa Ali alipotembelea banda la Maonesho la Kamisheni ya Utalii wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Utalii Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Maoneshi ya Kitalii Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, kufungua maonesho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar

Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Utalii Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia katika ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Kitalii Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar na kuhudhuriwa na Makampuni mbalimbali ya Kitalii ya nje na ndani ya Zanzibar.

122 thoughts on “Ufunguzi wa Maonesho ya Utalii Zanzibar Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama