Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tumieni Wataalamu wa Ndani Kuandaa Mipango Kabambe – Naibu Waziri Mabula

Na Munir Shemweta, SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ametoa rai kwa mamlaka za upangaji nchini kuandaa mipango kabambe ya maeneo yao kwa kutumia wataalamu washauri au wataalamu wa ndani kadri ya uwezo wa mamlaka husika.

Aidha, amezielekeza halmashauri ambazo zimeanzisha mchakato wa kuandaa Mipango Kabambe kuongeza jitihada kukamilisha kazi hizo na wataalamu watekeleze majukumu yao kwa weledi.

Naibu Waziri Mabula alitoa rai hiyo tarehe 19 Julai 2021 wilayani Sumbawanga wakati akizindua Mpango Kabambe wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

One thought on “Tumieni Wataalamu wa Ndani Kuandaa Mipango Kabambe – Naibu Waziri Mabula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama