Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TFDA Yangara Utoaji Huduma Bora Kwa Viwango vya Kimataifa

Na: Mwandishi Wetu

Mamalaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imetajwa kuwa na mifumo thabiti  ya udhibiti  iliyoiwezesha kutambulika na kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, na  kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hii.

Akizungumza katika Kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’  Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo  Bw. Adam Fimbo amesema kuwa  kutambulika kwa ubora wa huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo ni ishara kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikiiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“ Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.” Alisisitiza  Fimbo

Aliongeza kuwa  Mamlaka hiyo imeendelea kufanya jitihada za kuunga mkono  Tanzania ya viwanda ifikapo 2025, TFDA imekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada wa kiufundi na kuwajengea uwezo wenye  viwanda vya dawa nchini na kushawishi wawekezaji kujenga viwanda vya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba.

Akizungumzia mafanikio ya uhamasishaji ili wawekezaji wajitokeze kujenga viwanda vya dawa, Bw. Fimbo amesema kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji 70 wameonesha nia ya kuanzisha viwanda vya dawa ambapo viwanda vinne (4) vimeanza kujengwa.

Aidha, Bw. Fimbo amebainisha kuwa katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, Mamlaka ilitoa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa chakula 1,568 kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kukidhi matakwa ya kisheria ya usindikaji wa chakula salama.

Vile vile, TFDA imefuta ada za usajili wa majengo ya kusindikia chakula na ada za ukaguzi ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya ubora na usalama wa bidhaa wanazozalisha.

 Kwa kutumia mifumo hii, mwenendo wa utoaji wa vibali vya uingizaji na utoaji wa bidhaa nje ya nchi umeongezeka ambapo katika mwaka 2017/18, jumla ya vibali 11,866 sawa na ongezeko la 91% ukilinganisha na 13,018 mwaka 2016/17 vilitolewa.

Mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara

TFDA imeweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida na ISO 17025:2005 kwa huduma za maabara. Aidha, huduma za TFDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya Mkataba wa Huduma Wateja kama ulivyorejewa mwaka 2016.

Katika kuadhimisha miaka mitatu ya mafanikio ya utekelezaji wa kazi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.

 

86 thoughts on “TFDA Yangara Utoaji Huduma Bora Kwa Viwango vya Kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama