Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Kuendelea kuimarisha biashara na Malawi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali.

Na Fatma Salum-MAELEZO

Serikali ya Tanzania inaendelea na jitihada za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Serikali ya Malawi kupitia sekta ya biashara na uwekezaji ili wananchi waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika nchi zote mbili.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla alisema kuwa katika kuimarisha uhusiano huo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Malawi zimeandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Julai 26 na 27 mwaka huu Jijini Mbeya.

Makalla alieleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wan chi zote mbili ili kubaini fursa mbalimbali zitakazowezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda, usafirishaji, utalii, uvuvi, kilimo, madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, Tehama na biashara kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.

“Kongamano hili linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 500 ikijumuisha wafanyabiashara, wawekezaji, Taasisi za Umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Malawi,” alisema Makala.

Sambamba na kongamano hilo, kutakuwepo mikutano ya wafanyabiashara (B2B), mikutano ya watendaji wa Serikali (G2G) na mikutano kati ya Serikali na wafanyabiashara (B2G) kutoka nchi zote mbili.

Makalla alisisitiza kuwa Mkoa wa Mbeya uko tayari kuchangamkia fursa za kibiashara na Malawi kwa sababu miundombinu ipo ya kutosha ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, meli mbili za kubeba mizigo ambazo zimeshaanza kufanya kazi na meli moja ya abiria ambayo itakamilika Julai mwaka huu.

Baadhi ya watendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (hayupo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kuanza ujenzi wa kituo kimoja cha forodha (One Stop Boarder Post) katika mpaka wa Kasumulu na imetenga eneo la kujenga bandari kavu katika eneo la Inyala kwa lengo la kuwezesha upokeaji na uhifadhi wa bidhaa moja kwa moja kutoka bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Mnali alisisitiza kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa wafanyabiashara wa kitanzania hivyo wajitokeze kushiriki ili waweze kuibua fusra mpya na kujitangaza kwa wenzao wa Malawi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alitoa wito kwa wafanyabiashara wote hasa sekta binafsi kujitokeza kwa wingi kuangalia fursa zilizopo Malawi na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.

Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya Malawi (MITC) wanaratibu kongamano hilo na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Amos Makalla na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali.

(Picha na Eliphace Marwa – Maelezo)

6 thoughts on “Tanzania Kuendelea kuimarisha biashara na Malawi

 • October 27, 2020 at 2:28 am
  Permalink

  Your cash is being counted sildegra nedir 50 mg “It’s a success leads to further success scenario,” says Mark Hamrick, Washington bureau chief at Bankrate.com. “Until you see more impressive hiring numbers, it’s hard to imagine that a large number of people are going to jump back into the job market to think they stand a terrific chance of being hired.”

  Reply
 • October 27, 2020 at 4:30 am
  Permalink

  Could you give me some smaller notes? crestor prescription coupons “Edward Snowden’s actions were shocking and represented a grave violation of Booz Allen’s code of conduct and core values. As a result, he was immediately dismissed by the firm,” Fisher said. He said the company could not comment further due to the ongoing investigation of Snowden.

  Reply
 • October 27, 2020 at 7:59 am
  Permalink

  Do you know each other? seattle sutton coupons chicago Many of the places, stories and lives lived by New Yorkers who have come before us are still alive and well, but locked in photography archives. Check out these photos that blend places in New York Ci…

  Reply
 • October 27, 2020 at 10:51 am
  Permalink

  Best Site good looking decadron ovulos como usar The earnings season so far has been largely positive withmore than half of the companies that have reported beatingestimates. But cuts in outlooks from a number of bellwethers,including Intel and Caterpillar, mainly due toincreasing concerns over China’s growth, have raised fears aboutthe third and fourth quarters.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama