Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taifa Stars Yaitandika Botswana bao 2-0 Uwanja wa Uhuru DSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. George Harrison Mwakyembe akisalimiana na Waamuzi wa mpira kabla ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Botswana kuanza jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. George Harrison Mwakyembe akisalimiana na Kikosi cha Timu ya Taifa Stars hapo jana kabla ya mechi kati yao na Botswana kuanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. George Harrison Mwakyembe akisalimiana na Kikosi cha Timu yaBotswana hapo jana kabla ya mechi kati yao na Taifa Stars kuanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. George Harrison Mwakyembe pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shirikishola Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakisimama kuimba nyimbo za Taifa kabla ya mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Botswana kuanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Timu ya Taifa Stars kikipiga picha ya pamoja kabla ya mechi dhidi ya Botswana kuanza hapo jana katika Uwaja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Timu ya Botswana kikipiga picha ya pamoja kabla ya mechi dhidi ya Taifa Stars kuanza hapo jana katika Uwaja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kapteni wa Timu ya Taifa Stars Mbwana Samatta (mwenye jezi ya bluu) akiwatoka wachezaji wa timu ya Botswana kuelekea langoni mwa timu yao katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mchezaji nyota wa Timu ya Taifa Stars, Simon Msuva (katikati) akiachia shuti kali lililopelekea ushindi wa bao la kwanza wakati wa mechi kati yao na timu ya Botswana ambapo Taifa Stars iliibuka kidedea hapo jana kwa kuitandika timu ya Botswana mabao 2-0 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mashabiki waliokuwa wakiishangilia timu ya Taifa Stars hapo jana wakiwa wamefurika kushuhudia mpambano wa mechi hiyo kati ya Taifa Stars dhidi ya timu ya Botswana iliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuipelekea Taifa Stars kuwa washindi kwa mabao 2-0.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa ameketi kutazama mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Botswana iliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo Taifa Stars iliichapa timu ya Botswana mabao 2-0. Kulia ni Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Wallace Karia.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama