Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TADB Yaendelea Kuchagiza Mapinduzi ya Kilimo Katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga

Timu ya Ukaguzi ikiangalia mandhari ya mifereji inayotumia kumwagilia shamba hilo.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa mkopo unaotolewa na TADB.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54, mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa hekta moja.

Skimu hiyo ya Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo.

Timu ya Ukaguzi ikiangalia namna uongezaji wa thamani wa zao la mpunga unavyofanyika,

 

3 thoughts on “TADB Yaendelea Kuchagiza Mapinduzi ya Kilimo Katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama