Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taasisi za Elimu ya Juu Watakiwa Kutoa Elimu Itakayoboresha Maisha.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wanakikundi cha Bright Focus (hawapo pichani) wakati akifungua kikundi hicho kilichopo chuo cha Uhasibu Singida.

Na RS – SINGIDA

Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini zimetakiwa kutoa elimu itakayosaidia wahitimu kutambua fursa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati akizindua kikundi cha Bright Focus katika Chuo cha Uhasibu tawi la Singida chenye lengo la kutambua fursa za kuboresha maisha.

 “Natambua kuwa kikundi hiki kitasaidia kubuni mawazo yenye tija, fursa, na mwelekeo wa kuboresha uchumi miononi mwenu na kuelekezana namna bora ya matumizi ya rasilimali mlizonazo hususani rasilimali fedha,” alisema Dkt. Nchimbi.

Wanachuo ambao ni wanakikundi cha Bright Focus kilichopo Chuo cha Uhasibu Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kama ishara ya kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.

Makamu wa rais wa Bright Focus John Gama akiwasilisha malengo ya kikundi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi katika chuo cha Uhasibu Singida.

Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa mawazo ya wanakikundi yanapaswa kuendane na malengo ya kikundi hicho kuanzia mwenendo wa maisha, ufaulu na matumizi ya rasilimali yawe yenye muono wa kutengeneza faida na hasa kujifunza namna ya kuhifadhi akiba.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kikundi hicho, John Gama amesema kuwa kikundi kina malengo mengi ikiwemo kutoa udhamini kwa wanachuo ambao watashindwa kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali.

Ameongeza kuwa kikundi kitaanzisha miradi ya maendeleo kama vile kilimo, biashara ya bajaji na pikipiki, ufugaji wa nyuki na kuanzisha makapuni mbalimbali siku za baadaye kwa ajili ya kuongeze kipato kwa wanakikundi.

Vilevile kikundi hicho kina lengo la kutatua changamoto ya ukosefu wa uzoefu hasa linapokuja suala la ajira kwa kuwaajiri wanachuo katika makampuni watakayoanzisha ili waweze kupata ujuzi.

Kikundi cha Bright Focus kina jumla ya wanachama 89 ambao ni wanachuo, walimu na walezi wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, ambapo wamempendekeza Dk. Nchimbi kuwa mlezi wa Kikundi hicho.

76 thoughts on “Taasisi za Elimu ya Juu Watakiwa Kutoa Elimu Itakayoboresha Maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama