Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari.

Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu,wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa katika hafla ya futari aliyoiandaa katika makazi yake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Katika Hafla hiyo ya futari Mhe. Samia Suluhu Hassan alishiriki katika utoaji wa vyeti kwa wadau wa mazingira ambao walishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa tarehe 4 June, 2017,  Butiama mkoani Mara.

Baadhi ya taasisi zilizopatiwa vyeti na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ni Shirika la Utangazaji Tanzania- TBC, Clouds Media, Lake Gas limited, Tbl, Zantas Air na WWF.

Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuanda futari hiyo katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani amesema ni jambo zuri na linalompendeza Mwenyezi Mungu.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dar es Salaam

19-June-2017.

 

40 thoughts on “Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama