Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Mkuu Aongoza Maombolezo ya Kifo cha Katibu Mkuu wa CWT

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo alipo hudhuria msiba kwa aliyekua Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa, leo Novemba 18, 2017 nyumbani kwa marehemu Toangoma, jijini Dar es salaam. Aliye simama kwa kwa Waziri Mkuu ni Mke wake Mama Mary Majaliwa.

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma Jijini Dar es Salaam.

Bw. Msulwa  amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Bi. Sharifa Msulwa kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa . Waziri Mkuu alifika nyumbani kwa Marehmu Toangoma  jijini Dar es salam leo November 18, 2017.

Waziri Mkuu amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.

“Wote tumeguswa na msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa. Aaliye simama kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa  pamoja na Mke wake  leo Novemba 18, 2017 nyumbani kwa marehemu Toangoma, Jijini Dar es salaam

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.”

Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

JUMAMOSI, NOVEMBA 18, 2017.

108 thoughts on “TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama