Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Umma

Upimaji wa Magonjwa ya Moyo na Utoaji wa Elimu ya Afya ya Moyo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha Wahariri na Waandishi wa Habari kwamba katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani itafanya uzinduzi wa upimaji wa afya ambao utaenda sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wote pamoja na watoto wao. Upimaji huo utafanyika tarehe 28/09/2018 kuanzia saa nne (4) asubuhi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete. Usikose kuhudhuria nafasi hii muhimu ya upimaji wa afya.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inasema: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.

Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

27/09/2018

75 thoughts on “Taarifa kwa Umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama